Usiangalie Washindani Wako, Angalia Hadhira Yako Pale Unapotoa Ujumbe.

Kwa asili, sisi binadamu tunapenda ushindani, tunapenda kushinda na kuhakikisha tupo sahihi zaidi ya wengine. Lakini kitu pekee ambacho mtu anapata kwenye ushindani ni maumivu ya kichwa. Zaidi ya ufahari (ego) kwamba umeshinda, hakuna kingine bora unachopata kwenye ushindani zaidi ya kupoteza muda, nguvu na hata fedha.

Kwenye uandishi pia kumekuwa na ushindani mkubwa. Inawezekana wakajitokeza watu wanaopinga kile unachoandika, au wakaiga kile unachoandika wewe. Je unafanya nini kwenye hali kama hii?

Hatua ya kwanza kwa wengi ni kutaka kushindana, kutaka kuwakosoa, kuwaonesha kwamba wewe ndiyo upo sahihi na wao wanakosea. Lakini unajua hilo litapelekea nini? Wao kujitetea zaidi, na kukupinga zaidi, na hata wakiweza kukudhalilisha zaidi. Watakusumbua sana na watakutoa wewe kwenye mstari mzuri wa kuwapa wasomaji wako kile ambacho wanakipata kutoka kwako.

Ndiyo maana ninakuambia, usishindane wala kutaka kuwasahihisha wanaokupinga. Haijalishi unafanya nini kwenye hii dunia, wapo watu ambao watakupinga, wapo watakaokuiga. Lakini pia wapo watakaokukubali, na wapo wengine wala hata hawajali unafanya nini.

Hivyo wajibu wako wewe, ni kwenda na wale wanaokukubali, wape kile ambacho kinawasaidia, wawezesha kuwa na maisha bora zaidi na utanufaika kwa hilo.

SOMA;Usiandike Kwa Sababu Hizi, Utajipoteza Wewe Mwenyewe

Na kuhusu wanaoshindana na wewe na kukupinga, kuwa bora zaidi. Kila siku kuwa bora zaidi ya siku iliyopita, kila wakati piga hatua zaidi. Kuwa mbunifu na fanya mambo mapya na bora zaidi, hiyo yote kuhakikisha anayekufuatilia anapata kilicho bora. wanaoshindana watafika mahali na kuanguka wenyewe, wale wanaokupinga watafika hatua na kuchoka. Na wewe utasimama kama mshindi, bila ya kushindana moja kwa moja.

Usishindane na wala usitake kuwakosoa wengine, wasaidie watu na mara zote kuwa bora zaidi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Usiangalie Washindani Wako, Angalia Hadhira Yako Pale Unapotoa Ujumbe.

  1. Pingback: Kitu Pekee Unachopaswa Kufanya Kama Mwandishi Ni Kuwa Bora Zaidi Kila Siku. | MTAALAMU Network

Leave a Reply