Andika Kama Unavyoongea, Na Siyo Kama Unavyojibu Mtihani.

Njia ya kwanza na iliyozoeleka kwenye mawasiliano kwetu binadamu ni mazungumzo.

Mazungumzo yana njia fulani ya kuwafanya watu kufuatilia kinachozungumzwa na kuweza kuelewa vizuri.

Pia mzungumzaji anakuwa na njia za kuwafanya watu kuendelea kusikiliza bila ya kuchoka.

Lakini inapokuja kwenye maandishi, huwa yanawachosha wengi kutokana na kukosa ule mtiririko wa maongezi.

Wengi wanapoandika, huandika kama vile wanajibu mtihani au kuandika ripoti ya utafiti.

Hivyo msomaji anaposoma, anakosa ule mtiririko anaoupata kwenye maongezi na hilo humpelekea kushindwa kuendelea na usomaji.

Ili kuepuka hali hii, unahitaji kuwa unaandika kama unavyoongea.

Ndiyo, jinsi unavyoongea na wengine, na wakawa na hamasa ya kukusikiliza, ndivyo pia unavyopaswa kutengeneza mtiririko wa maandishi yako.

Usiandike kitu ambacho kinamchosha mtu kusoma, badala yake andika kitu ambacho kinampa mtu hamasa ya kuendelea.

SOMA;Njia Ya Uhakika Ya Kuondokana Na Hofu Ya Kuandika.

Tengeneza mtiririko mzuri ambapo msomaji anaweza kukufuatilia.

Jenga hoja zako hatua kwa hatua kuhakikisha msomaji anakufuatilia vizuri mpaka mwisho.

Muhimu zaidi, andika kwa lugha ya kuwasiliana na msomaji wako moja kwa moja.

Kwa chochote unachoandika, mwandikie msomaji wako moja kwa moja, kama vile unaongea naye ana kwa ana.

Kwa njia hii unachoandika kitamgusa moja kwa moja na kuweza kuchukua hatua.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

2 thoughts on “Andika Kama Unavyoongea, Na Siyo Kama Unavyojibu Mtihani.

  1. Pingback: Hicho Unachofikiri Ni Kidogo Na Cha Kawaida, Wapo Wengine Kitawasaidia Mno, Usiache Kuwashirikisha. | MTAALAMU Network

  2. Pingback: Siri Kuu Ya Mawasiliano Ya Binadamu Ambayo Unaweza Kuitumia Kufanikiwa Kwenye Uandishi. | MTAALAMU Network

Leave a Reply