Usiangalie Umepata Likes Ngapi, Angalia Umegusa Watu Wangapi.

Moja ya changamoto kubwa za kizazi chetu, ni kupima vitu kwa mzani ambao siyo sahihi.

Hebu fikiria, umeenda kupima uzito, halafu mpimaji akakuambia kwa sasa tuna kifaa cha kisasa ambacho kinapima uzito kwa wewe kusimama mbele ya kioo, halafu unaletewa uzito wako. Ukafanya hivyo kweli, na majibu yakaja, uzito wako ni sentimita 170, na mpimaji akakuambua uko vizuri sana. Utapokeaje matokeo hayo? Unapimwa uzito, majibu yamekuja kwa sentimita, umeambiwa upo vizuri, unashangalia na kusema safi kabisa, nipo vizuri, je utakuwa sawa?

Sasa turudi kwenye uandishi, je ni kazi ipi ya uandishi ina mafanikio katika zama hizi za teknolojia ya mitandao ya kijamii? Kuna mtu kaandika kitu fulani, watu wakiweka likes nyingi mno, na ikaishia hapo. Mwingine ameandika kitu kingine, amepata likes chache mno, lakini watu wawili wamemtafuta na kumwambia alichoandika kimekuwa na msaada kwao, wanamwambia hatua walizochukua na matokeo waliyopata. Je ipi kazi ya uandishi yenye mafanikio?

Unaweza kuona ni namna gani tunaishi kwenye mvurugano mkubwa mno. Tunatumia vipimo visivyo sahihi kupima kazi za uandishi. Tunaangalia tumepata likes ngapi, kama ni nyingi basi kazi yetu ina mafanikio, kama likes ni chache basi haina mafanikio.

Nimekuwa naona hili likiwaumiza waandishi wanaoanza, wanakata tamaa pale wanapoandika lakini hawaoni watu wakionesha wazi wazi kwamba wanapenda kazi zao. wanaona hakuna anayejali, wanakata tamaa na kuacha.

SOMA;Je Unawezaje Kuandika Kuhusu Mafanikio Iwapo Wewe Hujafanikiwa?

Lakini kwa uzoefu wangu binafsi, hakuna kazi ya uandishi inayoenda bure, hakuna kabisa. kuna mtu hata mmoja tu, ambaye anaichukua kazi yako na kuifanyia kazi, hataweka like leo, hatakutafuta, lakini atafanyia kazi. Na siku moja atakuja kukuambia, nimekuwa nasoma kazi zako siku nyingi, zimenisaidia sana.

Ninachotaka kukuambia hapa ni kwamba, usiache kuandika kwa sababu unapata likes chache, usiache kuwashirikisha watu mawazo yako kwa sababu hakuna wengi wanaokuunga mkono. Wakati mwingine kazi ya uandishi ni ya imani kama ilivyo kwa mkulima, anapanda mbegu ardhini, baadaye zinakuja kuota, hakupoteza mbegu zile. Hivyo wewe kama mwandishi, andika, unaweza kuona unaongea mwenyewe, lakini hakuna kinachopotea, ipo siku watu watakuambia kazi zako zimekuwa zinawasaidia, na hayo ndiyo mafanikio makubwa sana ya kazi ua uandishi.

Mafanikio ya kazi ya uandishi siyo likes, bali namna gani unawagusa wengine, namna gani unawapa maarifa sahihi yanayowawezesha kuchukua hatua, kuweza kufanya maamuzi sahihi na kuwa na maisha bora.

Ni vigumu mbo kupima mafanikio hayo kwa likes, coments na kata kushare. Wewe fanya kazi yako, kuwa na imani kama mkulima anapopanda mbegu ardhini, na wakati unapofika, mbegu hizo zinachipua na kuzaa matunda mengi zaidi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Usiangalie Umepata Likes Ngapi, Angalia Umegusa Watu Wangapi.

  1. Pingback: Saikolojia Ya Mitandao Ya Kijamii Inayowazuia Wengi Kuwa Na Blogu. | MTAALAMU Network

Leave a Reply