Usiwahadae Watu Kusoma, Utawapata Wengi, Lakini Hawatakuwa Muhimu Kwako.

Moja ya changamoto kubwa zinazoikumba sekta ya ujasiriamali wa habari, yaani kutoa taarifa na maarifa kwa njia ya mtandao, ni kuwepo kwa habari nyingi za uongo, zenye lengo la kupata wasomaji wengi.

Kumekuwa na kitu kinapigiwa kelele sana ambacho ni habari zisizo kweli yaani ‘fake news’ na kingine ni kupotosha kwenye kichwa cha habari ili mtu akimbilie kufungua, ambayo inaitwa ‘clickbait’.

Facebook-and-clickbait

Unaweza kutumia njia hizi kuwavutia wengi na kuwahadaa, huenda umeshaona wengi wakifanya hivyo. Kichwa cha habari kinakuvutia sana na unakimbilia kufungua, lakini ndani unakuta vilivyoandikwa ni tofauti kabisa.

Unaweza kushawishika kutumia njia hii kuongeza wasomaji wako kwa urahisi, lakini hili lina madhara makubwa sana kwako.

Kwanza kabisa utawafukuza wale watu makini ambao ndiyo muhimu kwako. Watu wakishakutana na hali hiyo, mara zote wanakumbuka huyu huwa anaandika vitu tofauti kwenye kichwa cha habari na ndani vitu vingine tofauti.

SOMA; Je Unawezaje Kuandika Kuhusu Mafanikio Iwapo Wewe Hujafanikiwa?

Pili utawakaribisha wale watu ambao siyo muhimu sana, wale ambao wapo tu kupata habari za udaku na uongo. Siyo watu ambao unaweza kuwapa maarifa sahihi na baadaye wakawa wateja wako.

Hivyo tumia njia sahihi ya kuongeza wasomaji wa kazi zako, kwa kutoa kazi bora na zinazowasaidia watu. Pia usitafute njia za mkato za kufikia wasomaji wengi, kua kwa hatua, kadiri unavyoboresha kazi zako, unavyotoa kazi nyingi zaidi, utaendelea kuongeza wateja zaidi.

Usidanganye wala kupotosha ili kupata wasomaji zaidi, unaweza kuona watembeleaji wanakuwa wengi, lakini watakuwa siyo watu makini.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply