Muda Wa Kuandika Upo Wa Kutosha, Ni Wewe Kusema NDIYO Na HAPANA.

Kwenye ujasiriamali wa taarifa, kazi kubwa sana unazopaswa kufanya ni mbili, kuandika na kusoma sana. Ninaposema sana namaanisha kweli SANA. unahitaji kuandika kila siku, wakati mwingine kuandika mara nyingi kwa siku moja. Lakini pia unahitaji kusoma ili kujifunza na kupata uelewa mkubwa kwenye kile unachoandika.

Hapa ndipo wengi wanapokwama, kwa sababu huona hawawezi kufanya hivyo, kutokana na kukosa muda kwa majukumu mengine ambayo tayari wanayo.

Huhitaji muda mwingi wa siku yako kuweza kufanya majukumu hayo mawili muhimu. Bali unahitaji angalau masaa mawili kwa siku. Saa moja ya kuandika na saa moja ya kusoma. Kadiri unavyokwenda unaweza kuongeza muda zaidi.

Sasa ukweli ni kwamba, muda huwa upo, kinachofanya muda ukosekane ni vipaumbele ambavyo tunaweka kwenye muda tulionao. Vile ambavyo umevipa kipaumbele kikubwa, ndiyo vinachukua muda wako mwingi.

time to write

Hii ina maana kwamba iwapo utaweka kuandika na kusoma kama kipaumbele kikubwa kwako, basi utapata muda wa kufanya hayo. Kwa sababu ukishaweka hayo kama kipaumbele, kuna ambayo unafanya sasa utahitaji kuacha kuyafanya.

Ni swala la kusema NDIYO kwenye kuandika na kusoma na kusema HAPANA kwenye mambo mengine unayofanya sasa ambayo siyo muhimu mno.

Hivyo ukiangalia kwa upande huo wa vipaumbele, swali siyo napata wapi muda wa kuandika na kusoma, swali linakuwa kipi muhimu kwangu zaidi ya kusoma na kuandika na kipi ambacho siyo muhimu.

Kinachowaponza wengi ni wanataka maisha waliyonayo sasa yaendelee hivyo hivyo bila ya kubadilika, halafu pia waweze kusoma na kuandika, kitu ambacho hakiwezi kutokea kabisa. Lazima uache baadhi ya vitu unavyofanya sasa, ili kuweza kupata muda wa kuandika na kusoma.

Hivyo basi, kuanzia sasa usiseme huna muda, bali sema wazi kabisa kile ambacho unajiambia huna muda wa kukifanya, ni siyo cha muhimu kwako kufanya. Kikishakuwa muhimu, muda upo na utakifanya.

Weka ujasiriamali wa taarifa kama kitu muhimu kwako na kila siku utapata muda wa kukuza ujasiriamali wako huo.

SOMA; Tenga Muda Wa Kutosha Kutangaza Kazi Yako Ya Uandishi, Hakuna Atakayekufanyia Hilo.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Muda Wa Kuandika Upo Wa Kutosha, Ni Wewe Kusema NDIYO Na HAPANA.

  1. Pingback: Uandishi Unaweza Kuwa Upweke, Hivi Ndivyo Unavyoweza Kupambana Nao. | MTAALAMU Network

Leave a Reply