Ubora Na Wingi Katika Uandishi, Kipi Cha Kuzingatia?

Katika uandishi, kuna njia mbili ambazo wengi hutumia kupima kazi zao.

Njia ya kwanza ni kuangalia wingi wa kazi, hapa unaangalia zile kazi unazotoa kwa namba. Kama ni makala basi unaangalia makala ngapi umeandika. Kama ni vitabu unaangalia vitabu vingapi. Kikubwa hapo ni wingi wa kazi ambazo mtu unatoa.

Njia ya pili ni kuangalia ubora wa kazi unazotoa. Hapa unaangalia kile ulichoandika kina ubora kiasi gani, watu wamekipokeaje, kimekuwa maarufu kiasi gani na vigezo vingine vya ubora.

Wingi na ubora vinaonekana kama kwenda kinyume. Yaani kaka kazi zikiwa nyingi basi ubora wake unashuka, na kama kazi zikiwa bora basi siyo nyingi.

wingi na ubora

Hii imekuwa inawafanya waandishi wengi kuamua kutoa kazi chache lakini bora.

Lakini tafiti na hata historia zinaenda kinyume kabisa na hilo. Ukiangalia waandishi ambao wametoa kazi bora kabisa tunazozikubali, walikuwa na kazi nyingi sana ambazo hazikuwa bora.

Hii ina maana kwamba, mwandishi anayeangalia kwenye wingi, katika kazi nyingi anazotoa, chache zitakuwa bora. lakini yule anayeangalia kwenye ubora pekee, anatoa kazi chache, na kwa bahati mbaya zinaweza zisiwe bora.

SOMA; Sababu Nyingine Kwa Nini Unapaswa Kuzalisha Kazi Nyingi Na Bora Zaidi.

Waandishi wengi wenye mafanikio wanakubaliana na dhana kwamba ni vigumu sana wewe mwandishi kupima ubora wa kazi kama ambavyo wasomaji au soko litapokea. Unaweza kuona kazi yako ni bora sana kwa vigezo vyako, lakini soko likapokea tofauti. Unaweza kuona kazi yako ni ya kawaida, lakini soko likaiona ni bora kabisa.

Hivyo ushauri kwa waandishi wote, badala ya kukazana na ubora na kuachana na wingi, tukazane na wingi huku tukizingatia ubora pia.

Kwa maana kwamba, kipaumbele chetu cha kwanza kiwe kutoa kazi nyingi tuwezavyo, na kwenye kila kazi tukazane kuweka ubora kadiri ya uwezo wetu. Halafu tuliachie soko lichague ipi kazi bora kwao.

Hii pia inakwenda kwa kila aina ya sanaa, kazi na hata biashara. Zalisha kwa wingi kwa ubora unaoweza kuzalisha, kisha soko litachagua kile kilicho bora kabisa.

Ukikazana kuangalia ubora pekee, utaacha kazi nyingi na itakuwa vigumu kwako kufikia ubora unaotaka kufikia.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply