Kuuza Kwa Uhaba Na Kuuza Kwa Mapenzi, Njia Bora Ya Kutumia Kupata Wanunuzi Wa Kazi Zako.

Uandishi kama zilivyo kazi nyingine, unahitaji wanunuzi, yaani watu ambao wanakubali kazi ya uandishi na kuwa tayari kulipia gharama ili kuipata.

Ubora wa kazi unachangia sana kwenye uuzaji, lakini kitu kingine muhimu kinachochangia ni uwezo wa uuzaji wa mwandishi. Kadiri mwandishi anavyoweza kuwafikia na kuwashawishi wapenzi wa kazi zake kununua, ndivyo anavyoweza kuuza zaidi.

buy books

Katika hili la ushawishi, zipo njia mbili ambazo zinaweza kutumika.

Njia ya kwanza ni hofu, hapa mwandishi anawashawishi wasomaji wa kazi zake kuchukua hatua ili kupata kazi ile kwa sababu wasipochukua hatua wataikosa. Hapa mwandishi anaweza kuweka ukomo wa muda wa kupata kazi zake hizo. Pia anaweza kutoa punguzo la bei ambalo ni la muda maalumu, ambapo watu wanapaswa kuchukua hatua katika muda huo.

Njia ya pili ni mapenzi, hapa mwandishi anatengeneza wasomaji ambao wanapenda sana kazi zake. Wasomaji ambao wanasubiri kwa hamu kila kazi ambayo mwandishi anaitoa. Wanakuwa tayari kulipia na  kupata kazi hiyo. Wasomaji wengine wanaweza kulipia kazi ambayo hata hawaihitaji sana, ila mapenzi yao kwa mwandishi yanawasukuma wao kufanya hivyo.

SOMA; Anza Kumwandikia Mtu Huyu Mmoja, Na Itakuwa Rahisi Kuwafikia Watu 1000.

Njia ya kwanza ni rahisi kutumia, inaweza kuleta wanunuzi wengi ndani ya muda mfupi kununua, lakini haiwezi kutengeneza wafuasi wazuri wa kazi zako za uandishi, au kazi zozote unazotaka kuwa na wanunuaji wa uhakika.

Njia ya pili ni ngumu, inahitaji muda na kazi kuweza kutengeneza wasomaji ambao wanapenda kazi zako na walio na kiu ya kupata kazi zako.

Njia ipi utumie wewe? Tumia njia zote mbili mwanzoni, ila mkazo weka kwenye kutengeneza wasomaji wanaopenda kile unachofanya. Hii itawafanya watu kukufuatilia na pia kuchukua hatua. Kwa sababu tabia zetu binadamu ni kutokuchukua hatua kwa haraka, mpaka tuone kuna kitu tunapoteza. Kadiri unavyokua, unaweza kuegemea upande wa mapenzi zaidi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply