Kila Wazo Linahitaji Kuboreshwa Zaidi, Hivyo Anzia Popote Na Endelea Kuwa Bora.

Moja ya vitu ambavyo vinawazuia watu kuchukua hatua, ni kutaka ukamilifu. Watu wengi wamekuwa wanajiona hawajakamilika hivyo kutokuanza, wanasubiri mpaka waone wapo tayari. Kitu ambacho huwa hakitokei.

Kitu kikubwa ambacho kinawafanya wengi kusubiri, ni kuamini kwamba bado hawajapata wazo bora kabisa kwao kufanyia kazi. Ni kawaida kwenye biashara, na hata kwenye uandishi na sanaa pia.

Mtu anakuwa anataka kuandika, iwe ni kitabu au makala, lakini hafanyi hivyo kwa kuona bado hajapata wazo zuri kabisa la kuandikia. Hivyo anasubiri mpaka apate wazo zuri kabisa ndiyo aandike. Kitu ambacho huwa hakitokei kabisa.

WriteYourStory

Kuondokana na hali hii, ili mtu uweze kuanza mara moja ni kujipa ruhusa.

Jipe ruhusa ya kuanza na wazo la kawaida sana, anza na kitu cha kawaida, lakini kazi yako kubwa ni moja, kuendelea kuwa bora zaidi.

Unaanza na wazo la kawaida, lakini unaendelea kukazana kuwa bora zaidi. Unakazana kuangalia maeneo ya kuboresha na kuchukua hatua.

Faida ya kutumia njia hii ni kujifunza kwa vitendo. Kwa mfano unapoanza na wazo la kawaida na kuendelea kujiboresha, utajifunza moja kwa moja kutoka kwa wale wanaopokea unachofanya.

SOMA; Kama Unasema Huna Muda Wa Kuandika, Nihakikishie Kwanza Hufanyi Vitu Hivi Vitano, Nitakuelewa.

Huenda mwanzoni ulifikiri watu wanataka kitu fulani, lakini unapokuja kufanya unagundua wanachotaka ni tofauti kabisa na ulichofikiri wewe, hivyo unahitajika kuboresha zaidi.

Ukisema usubiri mpaka upate wazo bora kabisa, utasubiri sana, na hata ukipata wazo hilo bado utahitaji kuliboresha pale unapoanza na kugundua watu wanahitaji tofauti na ulivyofikiri.

Kwa wale ambao wanaandika kitabu na hawajapata wazo zuri la kuandika, nimekuwa nawashauri kuanza na blog kwanza, kaundika kila siku kwa angalau siku 100 kisha kufanya tathmini, kwao wenyewe na kwa wasomaji wa makala zao. hapo wataona kipi ambacho wanaweza kufanya kwa ubora zaidi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply