Uandishi Unaweza Kuwa Upweke, Hivi Ndivyo Unavyoweza Kupambana Nao.

Ni raha kusoma kazi ya uandishi iliyokamilika, ambayo ni nzuri na ina maarifa na hamasa kubwa. Lakini kukamilisha kazi hiyo kunamgharimu mwandishi sehemu kubwa ya maisha yake.

Uandishi siyo kazi rahisi kama watu wengi wanavyofikiri, inahitaji nidhamu ya hali ya juu kukaa chini na kuandika, iwe ni makala, kitabu, ripoti na aina nyingine za uandishi.

Pamoja na uhitaji huo mkubwa wa nidhamu na kujitoa, kuna kitu kingine kinafanya uandishi uwe mgumu na wengi wasiupende. Kitu hicho ni upweke. Unapofanya kazi au biashara nyingine, mara kwa mara unakutana na watu wengine, iwe ni wafanyakazi wenzako au wateja, huchukui muda hujaongea na mtu mwingine au kuwasiliana na watu wengine.

Lakini kwenye uandishi, mambo ni tofauti. Huwezi kuandika huku unaongea na watu wengine. Huwezi kaundika huku unawasiliana na watu wakati huo huo.

andika kwa mapenzi

Kwa kifupi kwenye uandishi unahitaji kutenga muda wa kuwa wewe mwenyewe, na kupeleka mawazo yako kwenye kile unachoandika ili kutoa maarifa bora kabisa. Hata kama umezungukwa na watu wengine, utahitaji kujitoa na kuwa mwenyewe wakati unapoandika.

Hali hii inatengeneza upweke ambao wengine hawawezi kuuvumilia, wengi hawawezi hiyo hali ya kukaa wenyewe kwa muda ili kuandika.

Tunaishi kwenye dunia ambayo tumeshazoea kelele na usumbufu. Ndiyo maana kila mara tunataka kuangalia kwenye mitandao ya kijamii nini kinaendelea, tunataka kujibu kila ujumbe uliotumwa, kwa wakati uliotumwa, tunataka kila anayetupigia simu tupokee muda huo huo. Kwa kifupi tutafanya lolote ili kuepuka upweke.

SOMA; Muda Wa Kuandika Upo Wa Kutosha, Ni Wewe Kusema NDIYO Na HAPANA.

Lakini uandishi hautaki hivyo, unataka uwe wewe peke yako na mawazo yako, ili kuweza kuyapanga vizuri kwenye maandishi na yaweze kuwasaidia wengine.

Njia ya kuepuka upweke huu ili uweze kuandika vizuri ni kutenga vipindi vifupi vya muda wa kuandika. Unaweza kutenga nusu saa ya kuandika, ambapo kwa nunu saa hiyo hutaruhusu usumbufu wowote, simu itakuwa mbali, watu wengine hawatakusumbua. Uandike kwa muda huo, ukishaisha unaweza kuendelea na kelele nyingine.

Kama nusu saa ni kubwa kwako unaweza kuanza na muda mdogo zaidi ya hapo, muhimu ni uwe na muda tulivu ambao huruhusu usumbufu ili uweze kuandika. Kadiri unavyotengeneza muda wa aina hiyo na kuufanyia kazi, ndivyo unavyoweza kuukubali upweke wa muda, ukijua siyo wa kudumu.

Kila mtu anaweza kuvumilia kitu ambacho hakidumu kwa muda mrefu, tengeneza uvumilivu wa aina hiyo kwenye upweke wako wa uandishi, na utaweza kaundika zaidi. Unapopanga muda wa kaundika, kaa chini na andika, usiruhusu kelele yoyote ikutoe kwenye uandishi wako.

Kama nilivyowahi kukuandikia, uandishi ni mapenzi kabla hujafikiria kulipwa, na upweke huu ni sehemu ya mapenzi hayo.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply