Kuwa Wewe, Kuwa Halisi, Andika Kutoka Moyoni, Kile Unachojali Hasa.

Mitandao ya kijamii imeleta uharibifu mmoja mkubwa sana ambao ni watu kukazana kuishi maisha ya kuigiza. Watu wamekuwa wakikazana kuonekana wako vizuri kwenye mitandao ya kijamii wakati uhalisia wa maisha yao ni tofauti kabisa.

Hili lina athari kwenye maeneo mengi ya maisha yetu na moja ya maeneo hayo ni uandishi.

Unapoanza kuandika, watu watakuwa wanakujua kupitia uandishi wako. Wanavyokusoma, ndani ya akili zao watatengeneza picha yako. Kwa namna unavyoandika watu watategemea uwe mtu wa aina fulani, uwe na vitu fulani, uwe na misimamo fulani, ambayo huenda hata huioneshi kwenye uandishi wako.

kuwa halisi

Lakini kadiri wao wanavyokusoma, ndivyo wanavyotengeneza picha za namna gani wewe mwandishi upo. Sasa watu hawa wanapoanza kuwasiliana na wewe, na hata kukutana na wewe, utaona wanashangaa, ile picha walikuwa wamejijengea inakuwa tofauti na uhalisia waliokutana nao.

Utaona wanakuambia nilijua utakuwa mtu wa aina fulani, au nilijua utajua kitu fulani. Sasa hali hii imekuwa inawasukuma waandishi wengi kuishi maisha ya maigizo, kufanya vitu kwa vile wanavyotaka waonekane na siyo walivyo katika uhalisia.

Hii ni mbaya sana kwenye uandishi, kwa sababu kuishi maisha ya maigizo huwa kuna mwisho wake. Kuna wakati utachoka na kushindwa kuendelea kuigiza tena. Na mbaya zaidi, unapoigiza unawavuta watu ambao siyo halisi kwako, watu ambao hamuendani na hivyo hawatadumu na wewe.

SOMA; Kujitofautisha Na Wengine, Andika Na Kushauri Kile Unachofanyia Kazi Wewe Mwenyewe.

Andika kwa uhalisia wako, ishi uhalisia wako, hata kama siyo watu wanavyotegemea, lakini utapata kuridhika kutoka moyoni mwako. Na pia utawavutia wale ambao ni sahihi wako, wale wanaoamini kwenye kile unachoishi na unachoandika.

Na kwa kuwa uandishi ni kazi ya maisha yako yote, hutachoka kwa jambo lolote, kwa sababu hakuna maigizo, ni uhalisia mtupu.

Kuwa wewe, kuwa halisi na andika kutoka ndani ya moyo wako, huwezi kukubalika na kila mtu hivyo ni vyema ukamridhisha mtu muhimu sana kwako ambaye ni wewe mwenyewe.

Muhimu sana, hakikisha unalofanya ni jambo sahihi, usifanye jambo la hovyo na kusema ndiyo halisi kwako. Fanya lililo sahihi mara zote, na kazana kuwa bora zaidi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply