Category Archives: TENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO

Jinsi Unavyoweza Kutengeneza Pesa Kwenye Mtandao Wa Youtube.

Youtube ni mtandao unaompa kila mtu fursa ya kumiliki tv yake yeye mwenyewe, tena bure kabisa. kupitia youtube unaweza kuwa na chaneli yako kama ya tv, ambapo unaweza kuitangazia dunia chochote unachotaka, ila tu kiwe sahihi. Unaweza kurekodi video zako na dunia nzima ikaweza kuziona.

Watu wengi ambao wamekuwa wanaona chaneli za watu mbalimbali youtube, wamekuwa wakihamasika sana na wao kuwa na chanel zao, wakiamini ni njia rahisi kwao kujitengenezea kipato.

Wengi wanakimbilia kuanzisha chaneli zao, lakini mategemeo yao ya kutengeneza kipato yanazimika pale wanapokutana na uhalisia, kwamba kutengeneza kipato kupitia youtube siyo rahisi kama walivyokuwa wanafikiri.

Kupitia kipindi cha leo cha MTAALAMU NETWORK nimekufafanulia kwa kina jinsi unavyoweza kutengeneza kipato kupitia mtandao huu wa youtube. Nimekueleza kitu kimoja muhimu unachopaswa kukijenga kabla hujafikiria kutengeneza kipato. Hichi ni muhimu kufanyia kazi, kabla hata hujaanza kufikiria kulipwa. Ukiweza kufanyia kazi kitu hicho kimoja, utaona fursa za kutengeneza pesa zinakufuata zenyewe.

Baada ya kukamilisha kitu hicho kimoja muhimu, nimekushirikisha njia mbalimbali za kutengeneza kipato, na ipi unayoweza kuanza kutumia kulingana na hatua unayokuwa umefikia.

Wito wangu kwako ni uangalie kipindi hichi kama umewahi kufikiria kuhusu kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti na hasa mtandao wa youtube.

Kuangalia kipindi hichi, bonyeza maandishi haya. Pia unaweza kuangalia moja kwa moja hapo chini.

Fanyia kazi haya uliyojifunza kwenye kipindi hichi cha leo, weka juhudi kubwa katika kutoa maarifa na taarifa sahihi ili uweze kujitengenezea kipato kwenye mtandao wa intaneti.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

fb instagram

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Usitafute Fedha Za Haraka Mtandaoni, Utapoteza Muda Wako Na Kuharibu Uaminifu Wako.

Msingi mkuu wa kutengeneza fedha ni mmoja, na unafanya kazi iwe ni unapata fedha hizo shambani, kwenye ajira, kwenye biashara na hata kwenye mtandao; fedha ni zao la thamani unayozalisha kwa wengine.

Kama kuna kitu chochote unachoambiwa kinalipa, swali la kwanza kujiuliza je ni thamani gani unazalisha kwa wengine mpaka wakulipe? Ukijiuliza swali hili moja, kamwe hutatapeliwa wala kupoteza muda wako kwa mambo yasiyo sahihi.

Kutokana na ugeni wa mitandao na njia zake za kutengeneza kipato, watu wengi wamedanganywa na kuhadaiwa. Wanaambiwa wabonyeze link fulani au watume ujumbe fulani kwa watu wengi na watalipwa fedha.

getpaid_scam

Huo ni uongo mkubwa, unakupotezea muda na kusababisha usumbufu kwa wengine.

Ukweli ni kwamba unaweza kutengeneza fedha kwenye mtandao wa intaneti, lakini siyo zoezi rahisi kama wengi wanavyofikiri.

Hutakaa tu na kubonyeza link halafu ukapata fedha. Wala hutawatumia wengine link wabonyeze halafu wewe ukapata fedha.

Unahitaji kuweka kazi kubwa, kazi ya kuandaa na kutoa maarifa na taarifa ambazo zinawawezesha watu kuchukua hatua na kuboresha maisha yao. Waone thamani kubwa kupitia kile unachofanya, kisha wawe tayari kulipia huduma na bidhaa unazotoa.

SOMA; Jambo Pekee La Kiungwana Unaloweza Kufanya Kwenye Mtandao Wa Intaneti Ni Hili, Na Ukalipwa Pia.

Unahitaji kujifunza sana na kuwa tayari kuwafundisha wengine maarifa sahihi. Unahitaji kuyajua matatizo na mahitaji ya watu, kujua changamoto zao na kuweza kuwasaidia kuzitatua. Na wao kwa kuridhika na hilo, wawe tayari kukupa fedha zao, ili kupata zaidi.

Hivyo rafiki, unapoambiwa kuhusu njia mpya ya kutengeneza fedha kwenye mtandao, swali lako la kwanza liwe; ni thamani gani napaswa kutoa mpaka nilipwe?

Kama hakuna thamani unayopaswa kutoa, kama hakuna kazi unayopaswa kuweka, kimbia haraka sana, kuna watu wanataka kukutapeli.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Jinsi Ya Kuongeza Mauzo Ya Vitabu Kwa Waandishi.

Waandishi wengi wapya wa vitabu, huwa wanakutana na changamoto moja kubwa sana pale wanapotoa vitabu vyao vya kwanza. Changamoto hii huwa ni matarajio yao kutofikiwa.

Walichokuwa wanatarajia kabla ya kutoa kitabu, na wanachopata baada ya kutoa vitabu huwa tofauti kabisa.

fb instagram

Kabla ya kutoa vitabu waandishi huwa na matarajio makubwa sana. Huona uwezekano wa kuuza nakala nyingi za vitabu na kuwafikia wengi kwa haraka. Lakini wanapotoa kitabu, ndiyo wanakutana na ukweli kwamba hawawezi kufikia yale matarajio yao kwa haraka waliyokuwa nayo.

Katika kipindi cha leo, nimekushirikisha njia za kuweza kuongeza mauzo ya vitabu kwa waandishi.

Kwenye kipindi hichi nimezungumzia mambo matatu muhimu ambayo ni kutengeneza wasomaji wa kitabu kabla ya kutoa kitabu, kuweka mipango sahihi ya idadi ya vitabu na muda wa kuviuza na mwisho kutangaza kuhusu kitabu chako kupitia mitandao ya kijamii.

Angalia kipindi hichi cha leo, uweze kujifunza njia za kuongeza mauzo ya vitabu vyako.

Unaweza kuangalia kipindi hichi kwa kubonyeza maandishi haya, au kwa kuangalia moja kwa moja hapo chini kama kifaa chako kinaruhusu.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Matokeo Ya Kutangaza Biashara Kwenye Intaneti Hutayaona Haraka Kama Unavyotaka.

Kutangaza biashara kwa njia ya intaneti  ni kitu ambacho sasa kimeshaeleweka karibu na kila anayefanya biashara au kutoa huduma mbalimbali. Watumiaji wa intaneti ni wengi kutokana na simu zenye uwezo wa kuingia kwenye intaneti kuwa nyingi.

Pamoja na watu kuelewa na kutumia intaneti katika kutangaza biashara zao, wengi wamekuwa wakipata matokeo ambayo yanawakatisha tamaa.

Wengi wamekuwa wakiingia gharama kubwa kulipia matangazo kwenye mitandao mbalimbali mikubwa ambayo inatembelewa na watu wengi. Lakini matokeo ambayo wamekuwa wanayapata siyo kama walivyotegemea.

Huwa ni matokeo madogo sana ukilinganisha na matarajio yao.

mlm

Ukweli ambao kila mtu anapaswa kuuelewa ni kwamba, kutangaza biashara kwa njia ya intaneti hua hautoi majibu haraka kama wengi wanavyotegemea. Hivyo mtu anapaswa kuwa na uvumilivu mkubwa na kuendelea kutangaza hata kama mwanzoni haoni matokeo yoyote.

Mara nyingi watu wanaona tangazo, lakini hawachukui hatua kwa wakati huo, wanaliona tena wakati mwingine wanaweka kwenye kumbukumbu kwamba mtu huyu huwa anajihusisha na kitu fulani. Siku wakiwa na shida inayohusisha kitu kile, wanakutafuta moja kwa moja.

SOMA; Hii Ndiyo Njia Bora Kabisa Ya Kutangaza Biashara Yako Kwenye Mitandao Ya Kijamii.

Wafanyabiashara na watoa huduma wengi, wamekuwa wanataka wakitoa tangazo hapo hapo watu wengi wawatafute na kununua. Kitu ambacho hakiwezi kutokea kwa namna yoyote ile. Kuna mtu anaweza kuona matangazo yako mwaka mzima na asinunue chochote, lakini siku akiwa na shida inayohusiana na biashara yako atakutafuta.

Usikate tamaa pale unapotangaza lakini huoni matokeo mazuri. Wewe kazana kuboresha matangazo yako zaidi, yawe yanawalenga watu, kuwasaidia changamoto zao na kuwapa mahitaji yao.

Kazana pia kutengeneza hadithi ambazo zinawafanya watu kufikiria kuhusu wewe. Na inapofika siku wana uhitaji wa kile unachofanya, hawatasita kukutafuta wewe mara moja.

Matangazo ya kwenye intaneti hayatofautiani sana na matangazo ya kawaida, kama vile unavyoweza kuwa unaona bango fulani kwa muda mrefu, au tangazo fulani kwenye tv au redio kwa muda mrefu, hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye intaneti.

Ila kwenye intaneti unaweza kufanya hilo kwa ubora zaidi, kwa kuendelea kubadili na kuboresha tangazo kadiri muda unavyokwenda na namna wateja wanavyoulizia na kueleza changamoto au mahitaji yao.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Umuhimu Wa Kutangaza Kazi Zako Kwenye Mtandao Wa Intaneti.

Upo usemi kwamba kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza, huu ni usemi ambao umekuwa unatumiwa na wengi kama sababu ya kutotangaza kazi zao kwa nguvu.

Katika zama tunazoishi sasa, zama za mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii, unahitaji kutenga muda wa kutosha wa kutangaza kazi zako.

Iwe unafanya biashara au una kipaji kama cha uandishi, uimbaji, uchoraji na kadhalika, unahitaji kutumia mitandao ya kijamii kuwafikia watu wengi zaidi.

Hii ni kwa sababu kuna kelele nyingi mno, wapo watu wengi wanaosambaza maarifa mengi ambayo yanawazuia wale unaowalenga kujua kile unachowapatia. Hivyo tenga muda kutangaza kazi zako na itakulipa.

Zipo njia mbili za kutangaza kazi zako kwenye mitandao ya kijamii, moja ni ya kulipia na nyingine ni ya bure. Jinsi ya kutumia njia hizi nimeeleza kwa kina kwenye somo letu la leo.

Karibu ujifunze umuhimu wa kutangaza kazi zako na jinsi ya kufanya hivyo kwa kutumia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii. Angalia somo hili la leo kwa kubonyeza maandishi haya au kuangalia moja kwa moja hapo chini.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Watu Huwa Hawathamini Sana Vitu Vya Bure, Jifunze Kuweka Thamani Zaidi Na Kutoza Gharama.

Unapoanza kuingia kwenye ujasiriamali wa maarifa, kwa kutoa taarifa na maarifa kwa njia ya mtandao wa intaneti, vitu vingi utakuwa unatoa bure. Utaandika makala nyingi za bure, na huenda ukaandika vitabu na kuvitoa bure kwa wasomaji wako.

Hii ni njia nzuri ya kuwafanya watu wakujue na wajue kazi zako, kwa sababu ni vigumu kuanza kuwauzia watu ambao bado hawajakujua.

Lakini baada ya muda, unahitaji kujifunza kuweka thamani kubwa zaidi kwenye maarifa unayotoa na kisha kutoza gharama. Hii siyo kwa sababu tu unataka kutengeneza kipato, bali utawasaidia wengi zaidi.

paid-content-big1

Watu huwa hawathamini sana vitu vya bure. Kwa mfano kama umeandika kitabu na ukakitoa bure, ni wachache sana watakaokisoma mpaka mwisho. Wengi watakichukua na kukaa nacho, wakiamini siku wakipata muda watakisoma. Lakini muda huwa haupatikani.

Lakini iwapo utatoza gharama kwenye kitabu hicho, wengi watakaokinunua watalazimika kukisoma ili kupata thamani ya fedha walizolipia. Hii inawafanya wapate maarifa uliyotoa na kuweza kuyafanyia kazi.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuuza Maarifa Yanayopatikana Bure Kabisa Kwenye Mtandao.

Hili ni jambo muhimu sana unalopaswa kulifanyia kazi kwenye biashara yako ya kuuza maarifa, kwa sababu wengi wamekuwa wakivutiwa na kutoa vitu vingi vya bure na kushangaa mbona watu wanauliza maswali ambayo walipaswa kuwa wanayajua iwapo wangekuwa wamesoma ulichowaandikia.

Kuna tofauti kubwa kwenye kitu cha bure na cha kulipia. Toa maarifa mengi bure ili watu wakujue na kujua unawezaje kuwasaidia, lakini pia toa maarifa mengine ya thamani kubwa mno na toza gharama.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Kwenye Mitandao Ya Kijamii, Wewe Ndiyo Bidhaa, Hivyo Hakikisha Na Wewe Una Bidhaa Pia.

Wakati kampuni ya Facebook inanunua mtandao wa wasap kwa dola bilioni 19 (zaidi ya trilioni 40 za Tanzania), watu wengi walistushwa sana. wakati huo inanunuliwa, wasap ilikuwa na jengo moja la ofisi na wafanyakazi wasiozidi 20.

Swali kwa wengi lilikuwa mtandao huo ulikuwa na kipi kikubwa cha kuufanya uuzwe ghali kiasi hicho? Na jibu lilikuwa wazi, ulikuwa na watumiaji wengi, zaidi ya watu milioni 200 kwa kipindi hicho.

Hii inatuonesha wazi kwamba, kama unatumia mitandao ya kijamii, basi wewe ni bidhaa. Mitandao ile inakuuza wewe kwa watu mbalimbali ili kuweza kupata faida na kuendelea kujiendesha. Huwezi kulikwepa hilo, kama upo kwenye mtandao, jua wewe ni bidhaa.

Unauzwa kwa wanaotangaza biashara zao, unauzwa kwa wanaofanya tafiti na yeyote mwenye uhitaji wa watu kwenye mtandao, anaweza kuuziwa uwepo wako kwenye mtandao.

Kwa kuwa hatuwezi kukwepa hili, hatua pekee ya kufanya ni kuhakikisha na sisi kuna vitu tunauza kupitia mitandao hii. Kama wewe ni bidhaa, basi hakikisha pia una bidhaa ambayo inakuingizia wewe faida kupitia mitandao hii.

Kuwa na kitu, iwe ni huduma au bidhaa, ambayo unauza kupitia mitandao ya kijamii. Unawauzia watu moja kwa moja kwenye mtandao, kwa kutumia mtandao kama duka lako au njia yako ya kutangaza biashara yako.

Kila unapotumia mitandao ya kijamii, hakikisha kipo kitu ambacho unauza hata kama ni kidogo kiasi gani. Hii itakufanya wewe unufaike na mitandao hii na kuacha kuwa tu mteja au mtumiaji wa mwisho, ambaye unauzwa kwa wengine.

Uzuri ni kwamba, chochote ulichonacho, au unachopenda kufanya, unaweza kuwauzia wengine kwenye mitandao ya kijamii. Ujuzi wowote ulionao, uzoefu uliojijengea, vyote hivyo kuna watu wanavihitaji ili kuweza kuboresha maisha yao zaidi.

SOMA; Hichi Ndiyo Kitu Kinachowavutia Watu Kwenye Mitandao Ya Kijamii, Na Jinsi Ya Kukitumia Kutengeneza Kipato.

Angalia njia bora ya kuwasaidia kwenye hilo, iwe ni kupitia ushauri, vitabu na hata bidhaa nyingine zinazoweza kuwa za manufaa kwao.

Kama ungependa kujua njia bora kabisa kwako ya kutumia mitandao ya kijamii kwa faida, tuwasiliane kwa njia ya wasap namba 0717396253. Karibu sana.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Sababu Mbili Kwa Nini Watu Wapo Online Na Jinsi Ya Kuzitumia Kibiashara.

Unapotumia mtandao wa intaneti kama njia yako ya kutengeneza kipato, kupitia kazi zako mbalimbali, lazima uweze kujibu swali hili muhimu sana; kwa nini watu wapo online? Yaani nini kinawapelekea watu kuingia kwenye mtandao wa intaneti?

Na hili unaanza kulijibu kwa kuangalia tabia zako binafsi, kwa kuangalia kinachokufanya wewe uwe kwenye mtandao.

Kwa utafiti niliofanya, kuanzia mimi binafsi na watu wengine, zipo sababu kuu mbili kwa nini watu wapo online.

Sababu ya kwanza ni kupoteza muda.

Ndiyo, pamoja na umuhimu na uhaba wa muda, lakini hebu niambie unapotaka kupoteza muda unafanya nini? Unaingia kwenye mtandao wa intaneti, hasa mitandao ya kijamii, ukipanga kudhurura kwa dakika kadhaa. Labda ni mapumziko mafupi umepata kwenye kazi yako, au umefika wakati unataka kulala, unaweza kusema upitie kidogo mtandaoni kuangalia nini kinaendelea. Kwa kuwa kuangalia nini kinaendelea hakuna matokeo ya maana sana, basi ni kupoteza muda.

Unaweza kutumia hili kuhakikisha watu wanapoingia kupoteza muda basi wanakutana na wewe. Na hapa ni muhimu sana ujue watu wanapoteza zaidi muda kwenye mtandao katika nyakati zipi. Mara nyingi asubuhi kabla kazi hazijaanza, mchana wakati wa chakula na jioni baada ya kazi, watu wengi huwa kwenye mitandao. Hivyo unaweza kutumia muda huo kufanya kitu ambacho unataka kiwafikie wafuasi wako kwenye mitandao ya kijamii. Kama ni makala unaandika na kuwashirikisha watu, basi unapaswa kufanya hivyo wakati ambao watu wengi wanaweza kuiona. Japo hili siyo la uhakika sana, litakusaidia kuwafikia watu wengi zaidi.

SOMA;Usitangaze Biashara Yako Kwenye Blog Za Wengine, Badala Yake Fanya Hivi.

Sababu ya pili ni kutafuta njia ya kutatua tatizo.

Muda wowote unapokuwa na shida ni hatua ipi ya kwanza huwa unachukua? Kama kuna kitu unataka kujua au kujifunza, kwa dunia ya sasa, hatua ya kwanza ni google. Unatafuta taarifa za kitu hicho kwenye mtandao. Hivyo kutafuta njia ya kutatua tatizo fulani, ni sababu nyingine inayowapeleka watu online.

Kwa kujua hili, inakusaidia kujiweka kwenye mfumo ambao kila mwenye tatizo ambalo wewe unatatua, basi anakufikia wewe. Mtu anapoingia google na kutafuta kitu kinachohusiana na kile unafanya wewe, basi moja kwa moja aletwe kwako. Zamani kuna kitu kilikuwa kinaitwa SEARCH ENGINE OPTIMIZATION (SEO), ilikuwa ni njia ya kuweka maneno fulani fulani kwenye blog yako ili watu wakiyatafuta wafike kwenye blog yako. Mpaka sasa bado njia hiyo ipo, ila haina tena nguvu kama zamani. Na nguvu pekee iliyopo sasa, ni wewe kuwa na makala nyingi, na mpya mpya zaidi kuhusiana na kile ambacho mtu anatafuta. Mtandao wa google unapotafuta, unaangalia kwenye yale maeneo ambayo kitu kinachotafutwa kipo kwa wingi, na pia ni cha siku za karibuni. Hivyo unahitaji kuwa na makala nyingi zenye utatuzi wa matatizo ambayo watu wanatafuta suluhisho, na makala hizo ziwe mpya mara kwa mara.

Ukiweza kutumia njia hizi kuu mbili, kila wakati utawafikia watu wengi na wengi wakajua kazi zako na kununua kile ambacho unawauzia kupitia mtandao wa intaneti na blogu yako.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Jambo Pekee La Kiungwana Unaloweza Kufanya Kwenye Mtandao Wa Intaneti Ni Hili, Na Ukalipwa Pia.

Siku za nyuma, nilikuwa nasema kwamba huku Afrika, tumebaka teknolojia, hasa hii ya mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii. Nilikuwa nasema hivyo kwa sababu watu wengi walikuwa wanatumia mitandao hii bila ya kuwa na uelewa sahihi. Mtu anapata simu yake, anasaidiwa kujiunga na mitandao hii na kuanza kuitumia kama anajua vile. Hakukuwa na elimu yoyote ya matumizi sahihi.

Sasa ambacho kilikuwa kinatokea, ni watu kutukanana, kuzodoana, kukasirishana na hata kuvumishiana mambo yasiyo ya kweli. Hapo bado watu wengi walikuwa wakipoteza muda mwingi kwenye mitandao hii.

Nina hakika mpaka sasa wapo ambao wanaendelea na ubakaji huo wa mtandao, kwa kuutumia kwa hasara kwao na wale wanaowazunguka. Mtandao huu ni kitu kizuri lakini watu wanatumia kwa njia mbaya.

Sasa kwenye upande wa kutengeneza kipato, watu wanaendelea kubaka mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii. Wanakazana kufanya vitu bila ya kujua, na hilo linawapelekea kuchoka na kipato hawatengenezi. Wanakazana kuuza vitu kwenye mitandao, kutangaza sana, lakini hawapati wanunuaji wa kutosha.

Leo nakwenda kukuambia jambo moja la kiungwana ambalo unaweza kufanya kwenye mtandao wa intaneti, na likapelekea wewe kulipwa pia.

Jambo hilo ni kuwapa watu suluhisho la matatizo wanayopitia. Hili ni jambo la kiungwana sana, ambalo litawanufaisha watu, na kukunufaisha wewe pia.

Iko hivi, watu wana matatizo na changamoto wanazopitia kwenye maisha yao. Na wewe huenda ulishapitia matatizo kama hayo na ukaweza kutatua. Au una utaalamu unaoweza kuwasaidia watu hao. Au una uzoefu, kupitia wengine kwenye matatizo na changamoto hizo. Hivyo unachofanya ni wewe kuwashirikisha kile ambacho kinaweza kuwasaidia kutoka pale walipo.

Huhitaji elimu kubwa, huhitaji kuwa na fedha na wala huhitaji uwe na muda mwingi, ni wewe kuchagua kitu gani unaweza kuwasaidia watu kupata suluhisho, na kufanya hivyo.

SOMA;Sababu Moja Kwa Nini Wewe Unapaswa Kuwa Na Blog, Hata Kama Hutaki Kipato Mtandaoni (NA ZAWADI YA KITABU BURE.)

Unajuaje watu gani unaweza kuwasaidia?

Kama nilivyoeleza hapo juu, angalia mambo ambayo yanawasumbua wengine, lakini kwako ni rahisi. Angalia vitu ambavyo unajua wewe, lakini wengine hawajui. Halafu anza kuwasaidia watu kujua kile unachojua, kuwashirikisha njia bora za kuwatoa pale walipo.

Unawasaidia kwa njia gani?

Kwa kutumia akaunti zako za mitandao ya kijamii unayotumia, facebook, instagram, twitter, wasap na kadhalika.

Kwa kuwa na blog ambayo watu wanafika kujifunza zaidi, ambapo unaweka makala nzuri zaidi na huduma zako nyingine.

Na kwa kuwa na mfumo wa barua pepe (email list) ambapo unawasiliana na wasomaji wako na kuwapa zaidi lile suluhisho unalowaandalia.

Vitu hivyo vitatu lazima uwe navyo vyote, siyo kimoja, lazima vyote vitatu.

Kumbuka, kwenye mtandao wa intaneti, jambo la kiungwana kabisa kufanya, ni kuwasaidia watu kutatua changamoto wanazopitia.

Halafu sasa unaweza kuwauzia huduma zako zaidi, kama vitabu, ushauri, semina na kadhalika.

Kama unahitaji ushauri zaidi kwenye hili, tuwasiliane sasa kwa njia ya wasap 0717396253.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Kila Biashara Sasa Inahusisha Intaneti, Kama Bado Biashara Yako Haipo Kwenye Intaneti, Umechagua Kupoteza Wateja.

Kila wakati ambapo dunia inabadilika, huwa kuna watu hawayaamini mabadiliko hayo, na hivyo kuendelea kufanya kile ambacho walizoea kufanya. Kila teknolojia mpya inapokuja, wapo watu wanaoiangalia teknolojia hiyo kama kitu cha kupita pekee. Na wengi huona ni vitu vya vijana na siyo kwa watu wazima ambao wameshajenga misingi yao.

Lakini ipo fursa ambayo siyo tu ipo na kuendelea kuwepo, bali inaendelea kuwa kubwa kadiri siku zinavyokwenda. Yaani fursa hii inakua kwa kasi na kuzidi kuwa bora zaidi.

Fursa ninayoizungumzia ni mtandao wa intaneti.

Najua umekuwa unasoma makala nyingi ninazoandika kuhusu kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti, na labda unajiambia tayari nimeshajua hilo. Ninachokuambia ni kwamba bado hujajua, hakuna anayejua maana kila siku tunashangazwa na mtandao huu.

Kila siku kuna uvumbuzi mkubwa unagundulika kwenye matumizi ya mtandao huu, na watu wengi, wanajua labda asilimia 10 tu ya matumizi ya mtandao huu, ambapo ni kuwasiliana na wengine.

Hivi unajua ya kwamba kila biashara sasa, ndiyo nimesema kila biashara ni biashara inayohusisha mtandao wa intaneti?

Najua unaweza kusema hapana, kwa sababu labda biashara yako ni duka la mahitaji muhimu. Labda unauza vitu vidogo vidogo vya matumizi ya nyumbani. Na kuona kwa nini niwe kwenye mtandao, wakati wateja wangu ni watu waliopo kwenye mtaa wangu, ambao wakipita wanaona duka langu?

Nina swali moja kwako, je biashara hiyo ndiyo unapanga kuifanya maisha yako yote? Kweli unapanga maisha yako yote uwe na biashara ya duka la mahitaji ya nyumbani pekee? Kama jibu ni ndiyo basi unaweza kuishia hapa, kwa sababu hakuna kubwa utakalobeba hapa.

Lakini kama jibu lako ni kuwa mfanyabiashara mkubwa, zaidi ya hapo ulipo sasa, basi unahitaji kuanza kufikiria makubwa, na hapo mtandao wa intaneti ni muhimu sana kwako. Unahitaji kuanza kuitengeneza picha kubwa ya biashara yako kwa kutumia mtandao wa intaneti.

Unahitaji kuijua ndoto kubwa ya biashara yako, na kuangalia namna gani unaweza kufika pale, halafu uangalie jinsi gani unaweza kuanza kwa kutumia mtandao wa intaneti.

Kwa mfano kama ndoto yako ni kuuza vitu vya jumla baadaye, unaweza kuanza kwa kuwa na blog au tovuti ambayo inaelezea ile biashara ambayo unafanya au unapanga kufanya.

Unaweza kutumia blog au tovuti yako kama sehemu yako ya kuanzia, kwa kuonesha bidhaa unazouza na watu wakaweza kuziagiza moja kwa moja na ukawatumia. Kwa njia hii unaweza kuanza kidogo, bila hata kuwa na eneo kubwa la kuweka vile vitu unavyouza.

SOMA;Hivi Ndivyo Unavyoamua Kuwapoteza Wateja Wa Biashara Yako.

Pia unaweza kutumia mtandao wa intaneti kuwawezesha watu kufika kwenye biashara yako. Kwa kutumia blog yako kuwaelekeza ulipo. Au pia kutumia mtandao wa google kuiweka biashara yako kwenye ramani ambapo mtu akitafuta anaelekezwa.

Muhimu zaidi unaweza kutumia mtandao wa intaneti kuifuatilia biashara yako hata kama upo mbali na biashara yako. Unaweza kutengeneza mfumo wa kupiga mahesabu wa biashara yako ambapo ukiwa popote unaweza kufuatilia kila kinachoendelea kwenye biashara yako.

Kila unachofikiria kufanya biashara yako, kuna namna mtandao wa intaneti unavyoweza kukusaidia. Ni wewe kufanya utafiti na kuuliza maswali mazuri na utaweza kupata majibu sahihi ya kufanyia kazi.

Kila biashara sasa inahusisha mtandao wa intaneti, kama mpaka sasa hujaiweka biashara yako kwenye mtandao wa intaneti, au kama bado hujaweza kutumia teknolojia hizi mpya kuinufaisha biashara yako, tuwasiliane kwa wasap 0717396253 ili tuone namna gani unaweza kutumia fursa hii vizuri.